Monday, October 4, 2010

USIKU WA KANGA ZA KALEEE WAIVAAA!!!

JAMANI  MFANYE MUJE KUANGALIA SHOW ZA UKWELI, PATA PICHA SHAMIM JUKWAANI NACATWALK....JUU NA HIGH HEELS SI MIELEKA IYOOO.....UNAINGIA MWANZO WA STAJE HADI MWISHO NAANGUA KICHEKOOO....KWA KWELI ITAKUWA ZAIDI YA FASHION SHOW......MACELEBRITY WOOOTE WA BONGO KATIKA FANI YA MITINDO NA WADAU KUTOKA SEKTA MBALIMBALI SIKU HIYO NDO WATAKUWA JUKWAANI.....MAMODEL WATAKUWA WANATUPIGIA MAKOFI...PWA!! PWA!! PWAA!!
SI YA KUKOSA HIIIII!!!!

Saturday, October 2, 2010

USIKU WA KHANGA WAFANA DIAMOND JUBILEE

  Mwanamitindo Machachari Fiderin Iranga akipita na vazi la Khanga jukwaani katika onesho la Usiku wa Khanga onesho lililoandaliwa na mbunifu wa mavazi Asia Idarous kutoka kampuni ya Faback Fashion, onesho hilo linafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP usiku huu jijini Dar es salaam. Hivi sasa nahamia upande wa pili katika ukumbi huu huu wa Diambond Jubilee ambako kuna onesha la kukata na shoka la mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Ferre Golla (Shetani) ambaye anafanya onesho pamoja na bendi ya Mashujaa ya jijini Dar es salaam usiku huu.

Mbunifu wa mavazi kutoka kampuni ya Kapwani Grace Sinamtwa akiwa katika picha ya pamoja na Mathew aliyevaa shati lililobuniwa na mbunifu huyo.
Mwanamuziki Baby Madaha akiimba katika onesho hilo.
Mkurugenzi wa Casablanca Pub ya Kinondoni Mamaa Salma akiwa katika pozi.
Mbunifu wa Mavazi Grace Sinamtwa wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Jokate Mwegelo ambaye pia ameshiriki katika kuonesha mavazi ya Usiku wa Khanga kulia ni Brighter Fredy na kushoto ni Mathew Mkurugenzi wa Kapwani.
Wapenzi mbalimbali wa mitindo wakifuatilia onesho hilo.
Hebu licheki hili mdau
Vazi la jioni la kutokea lililobuniwa kwa khanga.
Vazi la ajabu lililobuniwa kwa makuti na Khanga.

mastaa watikisa jukwaa la usiku wa kanga za kale jana usiku Diamond Jublee


Mwimbaji mahiri wa taarabu hapa nchini,Khadija Kopa akiburudisha usiku huu kwenye usiku wa onesho la kanga za kale ambalo limefana kwa kiasi kikubwa,chini ya udhamini mkubwa wa bia ya Tusker.
Muaandaaji wa onesho la Kanga za kale Mama Asia Idarous Khamsini akikatiza jukwaani na Mumewe Mzee Khamsini kuwashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye onesho hilo usiku huu.
Mama Asia Idarous Khamsini akikatiza jukwaaani na baadhi ya mamodo waliovaa mavazi aliyoyabuni mbele ya wageni waalikwa.
Msataa mbalimbali walioshiriki katika onesho hili lilifana sana usiku huu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kuatiza jukwaaani na mavazi yao mbalimbali ya kanga.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Baby Madaha akiwa na madansa wakiwaburudisha wageni waalikwa waliofika kwenye usiku huu wa kanga za kale,ambali limefana kwa kiasi kikubwa.